TFF WAMKINGIA KIFUA MWAMUZI WA MECHI YA SIMBA NA YANGA
Wakti wadau mbalimbali wa mpira wa miguu hapa nchini wakiendelea kuhoji juu ya swala la mwamuzi aliyechezesha pambano la watani wa jadi Simba na Yanga Martin Saanya likishindwa kupatiwa ufumbuzi licha ya kuonekana amepindisha sheria 17 za soka,leo hii shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini limesema kwamba swala hilo bado linaendelea kufanyiwa uchunguzi hivyo ni vyema wadau hao wakawa watulivu ili vyombo husika vifanye kazi yake.
Ofsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba kwa sasa vyombo husika vinaendelea na uchunguzi juu ya jambo hilo na pia ni vyema watanzania wakafahamu kuwa waamuzi nao ni binadamu na si vizuri kuwauhukumu kwa haraka.
"Mimi nasema ni vyema wadau wa soka wakarejea kuutazama mpambano wa watani wa jadi na hasa kuangalia vizuri goli lililofungwa na Amisi Tambwe maana mwamuzi huenda kiuhalia labda hakuona kitendo cha kunawa pira kutokana na mahala alipkuwepo,hivyo si vizuri kutoa hukumu ya haraka"alisema Lucas.
Post a Comment