LICHA KUFUNGWA KWA JUMLA YA MABAO 30 KATIKA MECHI TATU KOCHA WA TWIGA STARS ATAKA ZANZIBAR IPONGEZWE

Baada ya timu ya wanawake ya Zanzibar,kuweka rekodi ya kua timu ya kwanza kufungwa idadi kubwa ya mabao katika michuano ya CECAFA inayoendelea kufanyika nchini Uganda,hatimae kocha mkuu wa timu ya Twigwa Stars Nasra Juma amesema kwamba licha kufungwa kwa idadi hiyo kubwa ya mabao lakini ni vyema pia timu hiyo ikapongezwa kwa hatua ambayo imefikiwa na timu hiyo.

Nasra amesema kwamba timu hiyo inashiriki michuano hiyo pasipo kua na maandalizi mazuri kama ilivyo kwa timu nyingine hivyo kufungwa kwa kwao kwa jumla ya mabao 30 ndani ya mechi tatu si jambo la kushangaza.

Katika hatua nyingine Nasra Juma amesema kwamba sababu nyingine ambayo imechangia timu ya wanawake ya Zanzabar kutofanya vizuri ni kutokana na matatizo yaliyopo kwa baadhi ya viongozi wa timu kushindwa kuwaruhusu wachezaji wao kujiunga na timu  kwa ajili ya mashindano hayo ya CECAFA ambayo ni ya kwanza kuanzishwa katika ukanda huu.

"Mfano mzuri ni kujitoa kwa wachezaji wa tano wa timu ya New Generation ambao wao walijitoa dakika za mwisho kabla ya safari eti kwa sababu ya viongozi wa timu hiyo kutoridhishwa na uwezo wa timu hiyo sasa nalo hili limekua tatizo na ni vyema viongozi wa ZFA wakalifanyia kazi jambo hili"alisema Nasra.

No comments