AKILIMALI AENDELEA KUMKATAA OBRY CHIRWA

 Katibu wa baraza la wazee wa Yanga Ibrahim Akilimali ameendelea kua na msimamo wake juu ya kutoridhishwa na kiwango cha mchezaji Obrey Chirwa ambapo amesema kwamba mchezaji huyo hakustahili kulipwa fedha ambazo amepewa katika usajili wake.

Amesema kwamba Chirwa ni mchezaji wa kawaida sana na na yeye ataendelea kupingana na wanaomshabikia mchezaji huyo juu ya kiwango chake kwani amekua hana msada kwa timu licha kupewa sifa kubwa wakati wa usajili wake.
 
"Nilipoanza kusema kuhusu kiwango chake watu wengi walinia juu lakini kwa sasa baadhi yao wanaanza kunipongeza juu ya mtazamo wangu,lakini ndugu Chirwa si mchezaji aliyestahili kulipwa kiasi kikubwa cha fedha kama alizopewa na kwa upande wangu nitaendelea kumkataa abadan"alisema Akilimali

Aidha amedai kua kwa sasa ni vyema mashabiki wa klabu hiyo wakaendelea kumuunga mkono kwani tayari ameshasaini kandarasi ya miaka miwili kwa kiwango kikubwa cha fedha,hivyo itakua kazi kubwa kwa uongozi kuvunja mkataba wake.

No comments