MAVUGO AENDELEA KUWAKOSHA MASHABIKI WA SIMBA


Mashabiki wa timu ya soka ya Simba wameendelea kufurahishwa na kiwango cha mshambuliaji wao Laudt Mavugo baada ya hii leo kuendelea kuifungia timu hiyo ya Simba katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo yeye alifunga goli la pili huku la kwanza likifungwa na Ibrahim Ajibu.

Wakiongea na MWANDIKE.BLOGSPORT mashabiki hao wamesema kwamba  kwa sasa hawana shaka na Mavugo juu ya kiwango chake kwani tayari kila mpenda soka anafahamu ubora wake hasa kwenye ufungaji.

"Ni kwambie mwandishi, Mavugo ni bonge la mchezaji na ataendelea kufunga kila wakati na hizi pia ni salamu kwa watani zetu Yanga kua wajiandae na kipigo,we si umeona kiwango chake kuna beki ambae ataweza kumzuia Mavugo asifunge pale Yanga"alisema shabiki wa Simba.


No comments