CHAMA CHA WUSHU TANZANIA CHAANDAA MASHINDANO YA TATU

Raisi wa chama cha mchezo wa Wushu hapa nchini Mwarami Mitete amesema kwamba chama hicho kimefanikiwa kuandaa mashindano ya tatu ya kimataifa ya mchezo huo yatakayofanyika siku ya jumamosi na jumapili katika uwanja wa ndani wa Taifa.

Mitete amesema kwamba dhumuni kubwa la kuandaa mashindano hayo ni kuhakikisha kwamba wanautangaza vyema mchezo huo ambao hapa nchini umekua hauna mwamko mkubwa.

Amesema kwamba chama hicho pia kimetoa mwaliko kwa vyama vya sanaa vya mapigano kujumuika kwenye mashindano hayo ambayo hayatakua na kiingilio.

No comments