MZOZO AMPONGEZA HANS POPE KWA KUMZAWADIA GARI TSHABALALA



Meneja wa mchezaji wa Simba Mohamed Hussein Tshabalala Henry Mzozo amemshukuru mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba,Zacharia Hans Pope kwa kutimiza ahadai yake ya kumkabidhi gali mchezaji huyo baada ya kuridhishwa na kiwango chake na nidhamu ya mchezo aliyokua nayo.

Mzozo amesema kwamba leo hii Hans Pope amefanya jambo jema ambalo linafaa kupongezwa hasa baada ya kutambua mchango wa mchezaji kwa jambo hilo litampa faraja kubwa mchezaji mwenyewe na kuendelea kuitumikia vyema timu ya Simba.

Amesema kwamba mbali na kumkabidhi gari aina ya Toyota Raum, pia amempa shilingi milioni moja fedha za Tanzania kwa ajili ya kumsaidia kununua mafuta ya gari hiyo.

Aidha amedai kua jambao ambalo limempa faraja ni kuona zawadi hiyo ya gari haihusiani na maswala ya mkataba wa mchezaji ambao mkataba wake Mohame Hussein wa kuitumikia Simba unamalizika msimu huu.

No comments