MAPUNDA ASEMA MPANGO WAKE WA KUREJEA NCHINI KENYA UPO PALEPALE

 Mlinda mlango wa Zamani aliyewai kuzitumikia timu za Yanga,Simba na Azam kwa hapa nchini,Ivo Mapunda amesema kwamba mchakato wake wa kuelekea nchini Kenya kwa ajili ya kucheza soka upo pale na anataraji kuelekea huko pindi ligi ya nchi hiyo itakapomalizika.

Mapunda amesema kwamba kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na uongozi wa klabu ya AFC Leoperd na kwa kiasi kikubwa mazungumzo yanaenda viuzuri hivyo baada ya ligi ya Kenya kumalizika anataraji kujiunga na klabu hiyo.

Amesema kwamba kwa sasa hana mpango wa kucheza soka hapa nyumbani licha baadhi ya timu kujalibu kuhitaji huduma yake lakini kwa upande wake hafikilii tena kuchezea timu yeyote hapa nchini.

No comments