MOROGORO YAWA BINGWA WA MICHUANO YA AIRTEL RISING STAR


Timu ya vijana ya mkoa wa Morogoro imefanikiwa kuwa mabingwa wa michuano ya Airtel Rising Star iliyofikia tamati leo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Ilala katika fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

 Michuano hiyo ya Airtel Rising Star ikiwa na lengo la kuibua vipaji imefungwa rasmi na waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye ambapo awali waziri mkuu Khasimu Majaliwa ndie alipaswa kuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa michuano hiyo yenye lengo la kuibua vipaji lakini ameshindwa kuwepo baada ya yeye kwenda kuwaona wahanga waliokumbwa na tetemeko la ardhi huko kanda ya Ziwa ambapo tetemeko hilo limesababisha vifo vya baadhi ya watu pamoja na kusababisha majeruhi mbalimbali.
 Akiongea wakati wa fainali hizo Nape ameipongeza kampuni ya simu ya mkoni ya Airetel kwa kuendelea kuendesha michuano ya Airtel Rising Star ambayo imekua msada mkubwa kwa timu za taifa hususani timu ya vijana ya Serengeti Boys ambapo idadi kubwa ya wachezaji wa timu hiyo wametoka kwenye michuano hiyo.

Amesema kwamba ni jambo la kuwapongeza kwa mchango wao mkubwa ambao wanauonyesha kwenye sekta ya michezo na ni vyema wadau mbalimbali wakawasapoti kwa namna mbalimbali ili waendelee kuwa na mashindano hayo yaliyofanyika kwa awamu ya sita hadi sasa.

"Serikali kwa upande wetu kwa sasa tunaangalia jinsi gani tunawasaidia hawa wenzetu kwenye mfumo wao wa biashara ili nawao wapate faida ili waendelee kupata hamasa ya kuendelea kufanya hiki wanachokifanya" alisema Nape.

No comments