NAPE KUTOA MILIONI MOJA KWA KILA GOLI LITAKALOFUNGWA NA SERENGETI BOYS KWENYE MECHI YA MWISHO DHIDI YA CONGO


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema kwamba Serikali ya Tanzania itaendelea kuisapoti timu ya Serengeti Boys katika mchezo wao wa marejeano dhidi ya Congo Brazavile baada ya mechi ya hii leo kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 3-2.

Nape amesema kwamba amefurahishwa na matokeo ambayo yamepatikana kwenye mechi ya leo hii na amewataka wachezaji wa Serengeti Boys kutokata tamaa hasa kuelekea mechi ya mwisho itakayoamua timu itayofuzu kucheza fainali za kombe la vijana barani Afrika huko nchini Madagasca.

Aidha Nape amewaahidi wachezaji wa timu hiyo kwamba atatoa kiasi cha shilingi milioni moja kwa kila goli ambalo litafungwa na mchezaji wa Serengiti Boys kwenye mechi ya marejeano hii ikiwa kama motisha kwa wachezaji.

"Nawaahidi kua kwanza hizi pesa zenu za leo ambazo mmeshinda mabao matatu ambazo ni shilingi milioni moja na laki tano kesho mtazipata na pia katika mechi ijayo kila goli mtakalofunga nitatoa shilingi milioni moja kwa hiyo msihofu nyinyi pambaneni najua mtafanikiwa" alisema Nape.

No comments