TFF YARIDHISHWA NA KIWANGO CHA WAAMUZI WA LIGI KUU YA TZ BARA

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limesema kwamba limelidhishwa na kiwango cha waamuzi ambao wamechezesha michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara tangu kuanza kwa ligi hiyo.

Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPORT,Ofsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba mbali na kuridhishwa na maamuzi ya waamuzi pia wamepongeza ushindani uliopo katika timu ambazo zinashiriki ligi kuu ya Tanzania bara kwani kila timu inacheza kwa kujituma na kupata matokeo wakiwa ugenini pasipo malalamiko yeyote kutoka kwa timu pinzani.

Amesema kwamba dhumuni kubwa la TFF ni kuona ligi kuu ya Tanzania bara inaendelea kua bora na kuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine.

"Kiukweli ligi ya msimu huu imeanza vizuri na waamuzi wamechezesha vizuri kwa mechi ambazo zimechezwa mwenyewe si unaona baadhi ya timu zimepata matokeo mazuri tena wakiwa ugenini,makosa madogo kwa waamuzi yapo na ikumbukwe kua nao ni binadamu"alisema Lucas.

No comments