MAJIMAJI MBIONI KUMREJESHA ONGALA,YAWATOA HOFU MASHABIKI JUU YA VIPIGO
Uongozi wa timu ya Majimaji ya mkoani Ruvuma
umewataka mashabiki wa klabu hiyo kutokata tamaa na mwenendo wa klabu hiyo
kwani wanaamini timu itarejea katika wakati mzuri hasa kuanzia mechi ijayo.
Mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo Salum Masamaki
ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT, kwamba kwa sasa benchi la ufundi linaendelea kuyafanyia kazi mapungufu
ambayo yameonekana kwenye mechi hizo walizocheza ili waanze vyema kwa kuibuka
na ushindi kwenye mechi yao ijayo dhidi ya Ndanda.
Masamaki amesema kwamba kwa sasa wanategemea kuwatumia
wachezaji wapya ambao hawajai kuonekana kutokana na kutokamilika kwa usajili
wao lakini kwa sasa jambo hilo limeshughulikiwa na wanastahili kuanza
kuwatumikia wana Lizombe wa Majimaji.
Aidha Masamaki amedai kua kwa sasa uongozi upo katika
mazungumza na kocha Kally Ongala ili arejee kuifundisha timu hiyo baada ya
kuwepo na matumaini ya kupata mdhamini kampuni ya GMS ambae atawasaidia kulipa mishahara ya
wachezaji na benchi la ufundi.
"Ujue baada ya wadhamini wetu Symbioni kujiondoa kuidhamini timu yetu hali imekua ngumu katika ulipaji wa mishara ikiwemo ya kocha Kally Ongala lkn siku ya alhamisi tunataraji kusaini mkata na kampuni ya GMS ambao watatudhani na ndio maana Ongala ameamua kurejea" alisema Masamaki.
Amesema kwamba kwa muda mrefu wamekua kwenye mazungumzo na
makocha mbalimbali kutoka jijini Dar es salaam akiwemo Suleiman Matola lkn
juhudi za kuwapata makocha hao zimekua ngumu kutokana na wengi wao kuhofia
kutopata stahiki zao kwa kua timu haina Mdhamini.
Post a Comment