BAKARI SHIME ATAMBA KUFANYA VIZURI KATIKA MECHI YAO DHIDI YA CONGO
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya vijana ya Serengeti Boys,Bakari Shime amesema kwamba kikosi cha timu hiyo kimerejea kutoka nchini Shelisheli kikiwa salama hakuna mchezaji yeyote ambae ni majeruhi zaidi ya uchovu wa safari.
Shime amesema kwamba kambi yao ya Shelili imekua na faida kubwa hasa kupata utulivu wa hali ya juu ambao umewasaidia kukijenga kikosi cha timu hiyo kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Congo Brazaville hapo siku ya jumapili ya september 18 mwaka huu.
Amesema kwamba kwa sasa kilichopo ni kuendelea kufanya maandalizi mazuri na jambo la faraja kwao ni kuona TFF imewaandalia mazingira mazuri ya kambi hapa nyumbani.
"Naamini mechi hizo mbili tutafanya vizuri kama sio ya nyumbani basi ya ugenini kwani kikosi kipo vizuri na mwenyewe unaona mazingira ya kambi tuliyopo kwa sasa maana lbd wengi hawakutegemea haya yaliyofanywa na TFF"alisema Shime.
Post a Comment