YANGA WATINGA TFF KUOMBA MECHI YA MTIBWA SUGAR ISOGEZWE MBELE
Na,Said Ally
Uongozi wa timu ya soka ya Yanga umesema kwamba kwa sasa wanajaribu kuwasiliana na TFF ili kuliomba shirikisho hilo kufanya mabadiliko ya mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Mtibwa Sugar,mchezo uliopangwa kuchezwa march 3 mkoani Morogoro.
Msemaji wa Yanga,Dismas Ten ameiambia Saidallymwandike.blogspot.com kwamba nia yao ni kuliomba shirikisho hilo kubadirisha ratiba ya mechi hiyo ili waweze kujiandaa vyema na mchezo wao wa klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Township Rollers ya nchini Botswana.
Ten alisema kwamba mchezo wao wa klabu bingwa ni mkubwa hivyo wanahitaji kupata muda wa kujiandaa vizuri kabla ya pambano hilo linalotarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam march 7 mwaka huu.
Alisema kwamba ratiba ya michezo yao ya ligi na FA ina wapa wakati mgumu kujiandaa vyema katika michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika hasa baada ya kupangwa kucheza mechi za karibu karibu tena katika mikoa tofauti.

Post a Comment