MAVUGO AACHWA SIMBA IKIWAFUATA GENDERMARIE

Simba inaondoka nchini leo saa 11 jioni kwa saa za Afrika Mashariki kuelekea nchini Djibout kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Gendermarie Nationale.
Mchezo huo utachezwa February 20 nchini Djibout huku Simba ikijivunia ushindi wa mabao 4-0 iliopata kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Uongozi wa Simba umetangaza majina ya wachezaji 20 akiwemo mshambuliaji John Bocco ambaye aliumia kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu dhidi ya Mwadui lakini pia katika msafara huo ameachwa mchezaji Laudt Mavugo anaelezwa ameachwa kwa sababu ya kutokuwa na kiwango kizuri kipindi hiki.
Wachezaji wengine wanaoondoka ni Aishi Manula, Emanuel Mseja, Mohamed Hussein, Mzamiru Yassin, Bukaba Paul Bundala, Emanuel okwi, Moses Kitandu, Shiza Kichuya, Nicholas Gyan, Erasto Nyoni, James Kotei, Shomari Kapombe, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude, Ally Shomari, Said Ndemla, Yusuph Mlipili, Juuko Murshid na Asante Kwasi.
Kikosi hicho kitaongozwa na Kocha Mkuu, Pierre Lechantre na Kocha msaidizi, Masoud Djuma na viongozi wengine wa klabu hiyo.
Endapo Simba itashinda mchezo huo itakutana na mshindi baina ya Green Buffalo ya Zambia au Al Masry ya Misri.

No comments