RAIS WA FIFA AWASILI NCHINI


Rais wa shirikiso la mpira duniani FIFA Giann Infantino amewasili nchini Tanzania leo alfajiri kwa ajili ya mkutano wa FIFA ambao utafanyika jijini Dar es salaam leo hii katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere.

Rais huyo amepokelewa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe,Rais wa Tff Wallace Karia na mwenyekiti wa BMT Leodger Tenga.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka TFF zinaeleza kuwa Infantino pia atakutana na Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Khasim Majaliwa baada ya Rais wa nchi Dkt John Pombe Magufuli kukabiliwa na majukumu ya kikazi akiwa nchini Uganda.

No comments