MBAO FC WASEMA WAPO KAMILI KUWAVAA SIMBA

Na Said Ally
Kocha mkuu wa timu ya Mbao FC,ya Ilemela mkoani Mwanza Etienne Ndayiragije amesema kwamba kikosi chake kimejipanga vyema kuwakabili Simba hapo siku ya jumatatu katika mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Ndayiragije ameiambia Saidallymwandike.blogsport.com kwamba kikosi chake kimewasili salama jijini Dar es salaam na kwa sasa kipo tayari kwa ajili ya ya pambano hilo litakalopigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Alisema kwamba mechi yao dhidi ya Simba itakuwa na ushindani wa hali ya juu lakini kwa upande wao wamejipanga kupambana ili wafanikiwe kupata ushindi ambao utawapeleka juu katika msimamo wa ligi.

Aidha Ndayiragije amewataka mashabiki wa soka hapa nchini kuondoa dhana inayoendelea kusemwa na wadau wa soka kuwa timu hiyo imekuwa ikitoa upinzani mkali kwa Simba na Yanga tofauti na timu nyingine.

Sisi tunapambana na kila timu iliyo katika ligi na tunafanya maandalizi sawa, sasa nashangaa kwa nini wanasema hivyo,sijui kama kuzikamia hizo timu zingenipa pointi 19 ambazo ninazo hivi sasa,alisema Ndayiragije.


No comments