KESI YA KINA MALINZI YAENDELEA KUPIGWA KALENDA

Na,Unique Maringo
Kesi ya aliyekuwa rasi wa TFF Jamali malinzi na wenzake  imeendelea kupigwa kalenda hadi machi mosi 2018 katika mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu baada ya wakili wa Serikali kutoka TAKUKURU LEONARD SWAY Kudai kuwa jalada lipo kwa DPP analipitia akimaliza atalirudisha mahakamani hapo.
Kesi hiyo ambayo imefika mbele ya Hakimu mkazi Mkuu WILBORD MASHAURI KATIIKA MAHAKAMA YA KISUTU kwa ajili ya kutajwa,wakili huyo  ameomba tarehe nyingine ya kutajwa.
 Wakili wa utetezi Abraham Senguji amedai mahakamani hapo kuwa  ni miezi 8 hadi sasa wateja wao wapo gerezani, hivyo anaomba upande wa mashtaka uharakishe upelelezi.
Baada ya kueleza hayo, Swai amedai kuwa hawacheleweshi upelelezi wa kesi hiyo kwa kusudi bali jalada lipo kwa DDP analipitia hivyo anaomba kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine.
Baada kueleza hayo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi March 1,2018 kwa ajili ya kutajwa.
Mbali na Malinzi, washtakiwa wengine ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Msiande Mwanga.

Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani, 375,418.

No comments