TOWNSHIP ROLLERS YAIFUATA YANGA

Timu ya Township Rollers ya nchini Botswana imefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika licha ya kufungwa kwa jumla ya mabao 2-1 na timu ya Elmelek ya Sudan.

Township Rollers imefanikiwa kusonga mbele kufuatia ushindi wa mabao 3-0 walioupata wakiwa nyumbani ambao umewafanya kuwa na faida ya mabao 4-2 baada ya mechi ya ugenini kufungwa 2-1.

Kwa matokeo hayo Sasa Township Rollers itamenyena na Yanga katika hatua inayofuata ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa ngazi ya vilabu.

No comments