YANGA WALALAMIKIA RATIBA YA MICHEZO YAO

Uongozi wa klabu Yanga umesema kwamba ratiba ya mchezo wao wa kombe la FA na ile ya ligi si rafiki kwao kutokana wachezaji kutopata muda wa kupumzika.

Katibu mkuu wa klabu ya Yanga,Charse Boniphace Mkwasa amesema kwamba mechi zao zimepangwa karibu karibu kitu ambacho kitaleta athari kwa wachezaji hasa kutokana na umbali wa mikoa ambayo wanatakiwa kwenda kucheza.

Alisema kwamba timu imerejea jana usiku mishale ya saa tatu kutoka Shelisheli na pia wanatakiwa kwenda Songea kucheza mchezo wa FA dhidi ya Majimaji kisha baada ya mchezo huo itawalazimu kusafiri hadi mkoani Mtwara kucheza mechi nyingine ya ligi na Ndanda.

Mkwasa alisema kwamba mbali na mchezo huo utakaopigwa mkoani Mtwara pia wanatakiwa kusafiri hadi mkoani Morogoro kucheza mchezo mwingine wa ligi na Mtibwa Sugar,mechi ambayo itapigwa March 3 mwaka huu.

Aidha alisema kwamba ni vyema TFF na bodi ya ligi wakaiangalia upya ratiba hiyo hasa kwa upande wao kwani mbali na michezo hiyo wanatakiwa kucheza mchezo wa klabu bingwa barani Afrika March 7 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

No comments