CHIRWA AFUNGUKA MADAI YA KUGOMA KWENDA SHELISHELI

Baada ya kuwepo uvumi kuhusiana na taarifa zinazomuhusu mchezaji Obrey Chirwa kuhitaji kiasi cha shilingi milioni 150 kwa ajili ya kusaini kandarasi mpya ndani ya klabu,leo hii mchezaji huyo ameamua kuweka bayana juu ya jambo hilo.

Chirwa ambae ameshindwa kuambatana na timu kwenda Shelisheli kwa ajili ya mchezo wa marejeano wa klabu bingwa barani Afrika dhidi ya St Louis amesema kwamba taarifa hizo si za kweli.

"Sijawahi kusema wala kumwambia mtu yeyote kuwa nataka 150M kwa ajili ya mkataba mpya, sipendezwi na namna wanavyonizushia,nadhani nia yao ni kunigombanisha na wapenzi wa Yanga.
.
Niliumia kwenye mchezo dhidi ya Majimaji ajabu wanasema nimegoma, huu ni upuuzi,mimi ni mchezaji wa Yanga, mimi na klabu ndiyo wenye kujua hatima yangu ya baadae,niacheni nicheze mpira". alisema Chirwa.

No comments