MPINZANI WA YANGA KUJULIKANA BAADAE

Baada ya kuwatoa St. Loius ya Shelisheli kwa ushindi wa jumla ya magoli 2-1, Yanga sasa itamvaa mshindi baina ya Township Rollers ya Botswana na El Merrikh ya Sudan zinazorudiana baadae hii Leo kunako mishale saa 2:30 usiku huko Sudan.

Mechi ya awali Rollers walishinda 3-0 katika mechi ambayo walikuwa nyumbani hivyo watakuwa na kibalua kigumu cha kulinda ushindi wao mbele ya El Merrikh.

Yanga Leo hii imesonga mbele kufuatia matokeo ya sale ya 1-1 matokeo ambayo yamekuwa mazuri kwao hasa baada ya mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salam kupata ushindi wa 1-0.

Bao la Yanga Leo hii limefungwa na Ibrahim Ajibu kunako dk ya 45 ya mchezo.

No comments