MBAO FC RASMI WAANZA KUMILIKI GARI

Mdhamini mkuu wa Mbao FC ya Ilemela mkoani Mwanza kampuni ya GF Trucks $ and Equipment leo hii imekabidhi basi kwa timu hiyo ambalo litatumika katika shughuli za timu.

Hafla ya makabidhiano hayo yalifanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Vingunguti Pugu Road na kuhudhuriwa na mgeni Rasmi Mheshimiwa Angeline Mabula ambae ni Naibu waziri wa ardhi na maendeleo ya makazi.

Mbao FC ilisaini mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya shilingi milioni 140 ambapo mgawanyo wa fedha hizo klabu ilipewa pesa shilingi milioni 70 huku kiasi kilichobaki ambacho ni milioni 70 ilinunuliwa gari ambayo wamekabidhiwa leo hii.

No comments