LWANDAMINA BADO YUPO YUPO SANA NDANI YA YANGA

Kaimu mwenyekiti wa klabu ya Yanga,Clement Sanga amesema kwamba uongozi wa klabu hiyo hauna nia ya kumfuta kazi kocha George Lwandamina kwani wameridhishwa na ufundishaji wake.

Sanga alisema kwamba ingawa baadhi ya wanachama na mashabiki wa klabu hiyo hawaridhishwi na ufundishaji wake lakini kama uongozi upo kinyume na mashabiki hao wakiamini kocha huyo anayo nafasi ya kuiongoza Yanga vizuri hivyo bado ataendelea kwa muda mrefu.

"Sisi Yanga tumekua katika kipindi cha mpito pindi ambacho pia mwenyekiti aliachia madaraka yake,ile sapoti ambayo tulikua nayo ilikua haipo kwa hiyo manaake tumeenda sisi wenyewe kama  wenyewe na tumeweza kujipanga upya na tumechewa kuanza maandalizi hivyo naamini kocha anayo nafasi ya kuendelea kukijenga kikosi na kupata matokeo mazuri"alisema Sanga.

No comments