LULU AITWA MAHAKAMANI KUJIBU MADAI YA KUMUUA KANUMBA

Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam inatarajia kuanza kusikiliza kesi ya mauaji bila kukusudia inayomkabili Mwigizaji wa filamu Elizabeth Michael maarufu kama Lulu siku ya October 19, 2017.

Lulu anakabiliwa na kesi hiyo akidaiwa kumuua Msanii mwenzake, Steven Kanumba bila kukusudia, kinyume cha Kifungu cha 195 cha Kanuni za Adhabu (PC), April 7, 2012, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican.

Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya kesi za mauaji ya bila kukusudia iliyotolewa na Mahakama Kuu, kesi ya Lulu itaanza kusikilizwa siku hiyo ya October 19, 2017 mbele ya Jaji Sam Rumanyika.

No comments