LAMECK NYAMBAYA ASEMA UCHAGUZI WA BODI YA LIGI ULIKUA WA HAKI

Mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF,Lameck Nyambaya amesema kwamba uchaguzi wa bodi ya ligi uliofanyika leo hii ulikua huru na wa haki kwa pande zote.

Nyambaya alisema kwamba uchaguzi wa leo ambao ulimuweka madarakani kaimu mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga kua mwenyekiti wa kamati ya bodi ya ligi baada ya kupata kura 10 dhidi ya 6 alizopata mpinzani wake Hamad Yahya ulikua uchaguzi mzuri ambao uliendeshwa kwa kufuata taratibu zote.

Alisema kwamba kilichopo kwa sasa ni vyema wadau wakawapa ushirikiano wa kutosha viongozi hao ili watimize majukumu yao kwa weledi na hatimae kuleta maendeleo ya mpira wa miguu.

Aidha Nyamba ambae pia ndie msimamizi mkuu wa kituo cha mkoa wa Dar es salaam alisema kwamba katika mkoa wake hadi kufikia sasa hakuna malalamiko yoyote ambayo yamejitokeza kwa timu shiriki kwa ligi mbalimbali.

Hata hivyo aliongeza kua klabu zote ambazo zimecheza katika kituo chake zimefanikiwa kupata mapato yao halali pasipo bughuza kutoka kwa wasimamizi na pia hata matokeo yaliyopatikana kwa timu hizo si ya kutatanisha kama ilivyo kwa baadhi ya mikoa mingine.

No comments