SIMBA WAMTANGAZA MRITHI WA JACKSON MAYANJA

Uongozi wa klabu ya Simba umemtambulisha rasmi Djuma Massoud mzaliwa wa Burundi kua ndie kocha msaidizi wa timu hiyo ya Simba anaerithi mikoba ya kocha Jackson Mayanga aliyejiondoa kwenye kikosi hicho kutokana na matatizo ya kifamilia.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii mkuu wa idara ya Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Manara alisema kwamba uongozi umeamua kumpa majuku hayo kocha Massoud baada ya kuridhishwa na taaruma yake pamoja na mafanikio ambayo ameyapata katika timu mbalimbali.

Djuma alikua kocha mkuu wa timu ya Rayon Sport ya nchini Rwanda ambayo aliisaidia timu hiyo kuchukua ubingwa wa ligi pamoja na yeye mwenyewe kubeba tuzo ya kocha bora.

No comments