JACKSON MAYANJA AMPONGEZA OKWI

Kocha msaidizi wa timu ya soka ya Simba Jackson Mayanja amesema kwamba pointi moja ambayo wameipata katika mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar ina faida kubwa kwa upande wao kwani imewarejesha kileleni katika msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Mayanja alisema kwamba mechi yao dhidi ya Mtibwa Sugar ilikua na ushindani wa hali ya juu hivyo kupata pointi moja kwao ni jambo zuri hasa ukiangalia goli lao la kusawazisha limepatikana dakika za mwisho.

Aidha Mayanja alimpongeza mchezaji Emmanuel Okwi kwa jitihada zake binafsi ambazo amezifanya na kuisadia timu yake kupata goli la kusawazisha baada ya kutumia vizuri mpira wa azabu ulioenda mojamoja langoni mwa Mtibwa Sugar.

Simba ilifanikiwa kupata alama moja baada ya kukomboa bao kwenye dakika za nyongeza za pambano hilo lilochezwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na kumalizika kwa timu hizo kufungana bao 1-1.

No comments