MAKONDA AWA MGENI RASMI KATIKA UFUNGUZI WA UWANJA WA JKT RUVU

Timu ya JKT RUVU,siku ya ijumaa ya terehe 22 ya mwezi huu itazindua uwanja wake wa michezo ya nyumbani ya ligi daraja la kwanza,uliopo Mbweni JKT jijini Dar es salaam.

Afisa Habari wa JKT RUVU,Costantine Masanja alisema kwamba uwanja huo umepewa jina la Meja Jenerali Michael Joseph Isamuhyo ambae ni mkuu wa JKT kwa sasa.

Masanja alisema kwamba mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kua mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paulo Makonda.

Aidha aliongeza kua uzinduzi huo utaambatana na mchezo wa ligi daraja la kwanza kati ya JKT RUVU na Ashanti United ikiwa ni mechi ya kwanza kuanza kuchezwa kwenye uwanja huo kwa timu za ligi daraja la kwanza na pia ratiba rasmi itaanza kuanzia mishale ya saa tano na nusu asubuhi.

No comments