YANGA WAPO KAMILI KUWAVAA NDANDA FC

Uongozi wa timu ya soka ya Yanga umesema kwamba kikosi chao kimejipanga kuwakabili Ndanda hapo kesho katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara unaotarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Afisa Habari wa timu hiyo,Dismas Ten alisema kwamba kiujumla hali ya kikosi ni nzuri hivyo ni jukumu la benchi la ufundi kuamua wachezaji watakaowatumia kwenye pambano hilo.

Alisema kwamba kuelekea katika mchezo huo wataendelea kumkosa mchezaji Amis Tambwa aliye majeruhi kwa muda mrefu lakini wachezaji wote waliosalia wako vizuri.

No comments