BAADA YA KUTOFANYA MAZOEZI KWA SIKU YA JANA UONGOZI YANGA WAELEZA SABABU

Uongozi wa timu ya soka ya Yanga umesema kwamba kikosi cha timu hiyo hakipo kwenye mgomo kama inavyoelezwa na wadau wa mpira wa miguu hapa nchini.

Afsa Habari msaidizi wa klabu ya Yanga,Godlsetn Anderson Chicharito ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba swala la mgomo kwa wachezaji halipo na leo hii mazoezi yaliendelea kwa wachezaji wote walio kwenye hali nzuri.

Alisema kwamba walishindwa kufanya mazoezi kwa siku ya jana baada ya kuwepo kwa kikao kilichowahusisha wachezaji pamoja na viongozi wa klabu katika kipindi cha muda wa mazoezi.

Hata hivyo Chicharito amewaomba mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuisapoti timu kuelekea katika mchezo wao ujao dhidi ya Ndanda hapo siku ya jumamosi ili kikosi kifanikiwe kufanya vizuri.

No comments