NAIBU WAZIRI ATEMBELEA KAMBI YA SERENGETI BOYS

Naibu waziri wa Habari,utamaduni,Sanaa na michezo Anastazia Wambura siku ya jana amefanikiwa kuitembelea kambi ya timu ya Taifa ya vijana ya Serengeti Boys inayojiandaa na ushiriki wa fainali za Afrika kwa vijana zitakazofanyika hapa nchini mwaka 2019.

Afsa Habari wa TFF,Alfred Lucas alisema kwamba ujio wa naibu waziri umekua na tija kubwa kwa kikosi cha timu hiyo hasa katika maandalizi ya timu kuelekea kwenye fainali hizo.

Alisema kwamba baada ya kuwasili katika kambi hiyo amejionea hali halisi ya kambi kwa ujumla huku pia akiridhishwa na mipango iliyokuwepo katika timu hiyo akiamini kua Tanzania itafanikiwa kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.

No comments