YANGA WAMFUATA MANJI MAHAKAMANI

Na Unique Maringo
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imehairisha kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin inayomkabili mfanyabiashara Yusufu Manji.

Wakili wa utetezi Hajra Mungula mbele Hakimu  Mfawidhi Cyprian Mkeha alieza kuwa kesi hiyo imekuja kwaajili ya kusikilizwa na wako tayari.

Alidai  kuwa mteja wake anahitaji kutoka kwa ajili ya matibabu kwasababu yuko nje kwa dhamana, aliomba mahakama kesi hiyo iweze kusikilizwa  siku tatu mfululizo.

Kwa upande wake Wakili wa serikali Timon Vitalis alidai kuwa anataka kusafiri mchana na hatoweza kusikiliza kesi hiyo.

Hakimu Mkeha alisema kuwa anakwenda kwenye kikao na kuahirisha shauri hilo ambalo litasikilizwa siku tatu mfululizo kwanzia Septemba 25 hadi 27.

Inadaiwa kuwa,kati ya Februari 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga Sea View Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin.

Kesi hiyo ipo katika hatua za usikilizwaji wa mashahidi upande wa utetezi ambapo shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, Mkugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof.Mohamed Janabi aliieleza mahakama kuwa Manji ana Vyuma kwenye moyo.

Baada ya kesi hiyo kuahirishwa  nje ya Mahakama Manji alisalimiana na mashabiki wa klabu ya Yanga waliokua mahakamani hapo pamoja na mchezaji wa timu hiyo Nadr Haroub maalufu kwa jina la Canavaro.

Mbali na Canavaro pia benchi la ufundi la Yanga likiongozwa na kocha George Lwandamina nao walihudhuria mahakamani hapo katika kesi inayomkabili aliyekua mwenyekiti wa klabu ya Yanga.

No comments