PROFESAR JAY AMPA SHAVU DIAMOND

Na Rodger
Moja kati ya Story ambazo zilikuwa zikitrend midomoni mwa watu na kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusiana na mtoto wa mwanamitindo nchini Hamisa Mobeto ambapo mtoto huyo alikuwa akihusishwa na mwanamuziki Diamond Platnumz AkA Chibu Dangote.

Sasa leo kupitia kipind cha Leo Tena Cha Clouds fm Diamond Platnumz amefunguka ukweli na uwazi juu ya mtoto huyo kuwa ni wakwake na ikumbukwe hapo awali Diamond Platnumz alikuwa akiuulizwa kama anatoka kimapenzi na Hamisa lakini alikuwa akikana.

Kutokana na uamuzi huo wa Diamond Platnumz kukubali kuwa mtoto huyo ni wake,baadhi ya wasanii wenzake wampongeza kwa uamuzi huo akiwemo Legend wa mziki wa Hip Hop nchini na Mbunge wa Jimbo la Mikumi Joseph Haule aka Profesar Jay,kupitia ukurasa wa Instagram Profesar Jay ameandika:

“Ukweli humuweka mtu huru KWELIKWELI..Big up Mdogo wangu @diamond platinumz umekuwa mfano bora sana.”

No comments