NJOMBE MJI WATAKA MATOKEO YA USHINDI

Uongozi wa klabu ya Njombe Mji Fc umesema matokeo ya ushindi uwanjani ndiyo kiu kubwa ya mashabiki na wapenzi wa timu hiyo, licha ya kufahamu mpira una matokeo matatu uwanjani.

Msemaji wa Njombe Mji Fc, Solanus Mhagama  ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba pamoja na klabu yao hivi sasa kuwa chini ya kocha Msaidizi Mrage Kabange ambaye anakaimu nafasi ya aliyekuwa Kocha Mkuu, Hassan Banyai kujiuzulu, mashabiki wa Njombe Mji wanahitaji timu yao ifanye vizuri katika michezo ya Ligi Kuu inayoendelea hivi sasa.

Alisema Njombe Mji Fc kwa sasa bado inasafari ndefu sana ya kufanya vyema katika soka licha ya kuwepo kwa changamoto nyingi zinazoikabili timu hiyo, ikiwemo kuendelea kutoa elimu kwa wadau na wafanyabiashara mbalimbali mkoani Njombe kuwataka waufahamu vyema mchezo wa mpira wa miguu na faida yake.

No comments