TFF KUWABAINI WANAOTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU KWENYE MECHI YA SIMBA NA YANGA

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limesema kwamba litawapima wachezaji wa Yanga na Simba kabla ya mchezo wa ngao ya jamii unaotarajiwa kupigwa agost 23 mwaka huu ili kubaini kama kuna baadhi ya wachezaji wa timu hizo huenda wakatumia dawa za kuongeza nguvu michezoni.

Afsa Habari wa TFF,Alfred Lucas alisema kwamba jambo hilo huwa linafanyika kwa timu zote zinazoshiriki ligi ya TFF,hivyo kuendelea kufanya hivyo ni sawa na mwendelezo wa swala hilo.

Lucas alisema kwamba upimaji huo utasimamiwa naTFF na madaktari watafanya jambo hilo kwa kuchukua vipimo vya mchezaji yoyote watakaemuhitaji kutoka kwa kila timu.

No comments