REAL MADRID YAICHAKAZA BARCELONA

Fainali ya SPAIN SUPER CUP kati ya REAL MADRID na BARCELONA imepigwa usiku wa kuamkia leo hii ikiwa ni EL CLASSICO nyingine  huku REAL MADRID ikiibuka mbabe wa pambano hilo lililopigwa nchini Hispania.

Mchezo ulionekana mgumu kwa pande zote huku watu wakitaka kuona Barca watakuwaje bila Neymar na dakika ya 50 mlinzi wa Barca Gerrard Pique aliipatia Madrid bao la kuongoza baada ya kujifunga.

Dakika ya 77 Lioneil Messi aliipatia Barca bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penati lakini dakika ya 80 Ronaldo aliipatia Madrid bao la 2 kabla ya dakika ya 82 kupewa kadi nyekundu na dakika ya 90 Asensio aliiandikia Madrid bao la 3.
Ronaldo, aliyeingia kama nguvu mpya alirejesha Real Madrid mbele alipokimbia kutoka katikati ya uwanja na kufunga.
Alipewa kadi ya njano kwa kuvua shati lake kusherehekea goli hilo lakini Muda mfupi baadaye, alioneshwa kadi nyingine ya manjano kwa kujiangusha na kutolewa uwanjani katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani wa hali ya juu.

Nako nchini Ufaransa mshambuliaji mpya wa PSG, NEYMAR ameanza kuifungia PSG katika ushindi wa mabao 3 dhidi ya
GUNGAMP huku mabao mengine ya PSG Yakifungwa na EDSON CAVANNI na JORDAN IKOKO akijifunga.

No comments