YANGA WADAI TSHISHIMBI ALIKUWEPO HAPA NCHINI

Wakati kukiwa na taarifa kwamba mchezaji Papy Kabamba Tshishimb ameungana na wenzake leo hii huko Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Simba hapo agost 23 mwaka huu,leo hii uongozi wa Yanga umesema kwamba mchezaji huyo hakuwasili leo hii kama inavyoelezwa.

Afsa Habari msaidizi wa Yanga,Godlisten Anderson Chicharito ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba Tshishimbi alikuwepo hapa nchini tangu wiki iliyopita na tayari ameungana na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.

Chicharito aliongeza kuwa kikosi cha timu hiyo kinaendelea vyema na maandalizi kikiwa Unguja na jambo la faraja ni kwamba wachezaji wote waliopo kambini wako vizuri kwa ajili ya pambano hilo.

No comments