TETESI ZA USAJILI ULAYA

Chelsea wanafikiria kutaka kumsajili mchezaji anayenyatiwa na Manchester United Ivan Perisic, 28, kutoka Inter Milan. (Mirror)
Barcelona wanataka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 26. (Diario Gol)
Cezar Azpilicueta, 27, anadhani Chelsea wanahitaji kusajili wachezaji kadhaa zaidi kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Evening Standard)
Chelsea wapo tayari kupanda dau la pauni milioni 50 wiki hii kumtaka beki wa kati wa Southampton Virgil van Dijk na kuwapiku Liverpool. (Daily Star)


    Manchester United watakuwa tayari kulipa pauni milioni 36.5 kumsajili kiungo wa Barcelona Sergi Roberto, 25, ikiwa mchezaji huyo atataka kuondoka Uhispania. (Don Balon)
    Manchester United wanakaribia kufikia makubaliano na Oliveirense ya Ureno kumsajili mshambuliaji Bruno Amorim, 19. (Daily Mail)
    Antoinne Griezmann, 26, atachukizwa na hatua ya Atletico Madrid kumuuza kipa wake Jan Oblak na huenda akafikiria kuhamia Manchester United. (Don Ballon)
    Leicester City watakataa dau la Roma la pauni milioni 31 la kumtaka Rirad Mahrez. Leicester wanataka pauni milioni 50. (Mirror)
    Mkurugenzi mkuu wa Juventus Beppe Marotta amesema wanamtaka kiungo anayesakwa na Liverpool Naby Keita, 22, anayechezea RB Leipzig. (La Gazzetta dello Sport)
    Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema anahitaji kuimarisha kikosi chake kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Liverpool Echo)
    Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anafikiria kumsajili mshambuliaji wa Napoli Lorenzo Insigne, kuchukua nafasi ya Philippe Coutinho anayenyatiwa na Barcelona. (Express)

    No comments