RT WAMUOMBA MAGUFULI AWAPE ENEO

Katibu mkuu wa chama cha mchezo wa Riadha Tanzania RT,Wilhelm Gidabuday amesema kwamba kupitia mashindano ya dunia ya riadha yalifonyika London Uingereza kwa upande wao kama chama wamejifunza mengi zaidi ambayo kama watayafanyia kazi yataleta chachu ya maendeleo.

Gidabuday alisema kwamba kupitia mashindano hayo wametambua umuhimu wa serikali  kupenda michezo ambapo amebaini kuwa nchi za wenzetu wanafanikiwa kwenye sekta kutokana na serikali zao kupenda michezo sambamba na kuwekeza katika sehemu hiyo.

Aidha alisema kwamba kwa upande wake kama katibu wa chama cha mchezo wa Riadha anamuomba Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,John Pombe Magufuli awape eneo la kutosha ambalo litawafanya kukamilisha mipango yao waliyojiwekea.

Alisema kwamba endapo jambo hilo litatimizwa anaamini kupitia wanariadha watakuwa na mchango mkubwa wa kuvitangaza vivutio vyetu vya nchi.



No comments