UONGOZI WA YANGA WATOA UFAFANUZI JUU YA SWALA LA KUPIGWA MNADA KWA JENGO LAO

Uongozi wa timu ya Yanga umewataka wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kutokuwa na hofu yeyote juu ya taarifa za jengo la klabu hiyo kuwepo kwenye mchakato wa kupigwa mnada baada ya kudaiwa kodi ya ardhi.

Katibu mkuu wa klabu ya Yanga,Charse Boniphace Mkwasa ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba ni kweli klabu hiyo inadaiwa kodi ya ardhi lakini uongozi tayari ushaanza mchakato wa kulilipa deni hilo.

Mkwasa alisema kwamba uongozi una vielelezo vyote juu ya swala hilo ambapo walishafanya mawasiliano na idara husika katika maswala ya ulipaji baada ya kukubaliana kuwa watalipa kidogokidogo kupitia fedha zao za mapato ya mechi.

Aidha alisema kwamba uongozi umeshangazwa na taarifa hiyo ya kutaka kupigwa mnada jengo hilo baada ya kampuni iliyopewa tenda hiyo kutangaza kuwa agost 13 jengo hilo litapigwa mnada baada ya klabu kudaiwa shilingi milioni 300.

No comments