VIONGOZI WA SIMBA KUIKOSA MECHI YA WATANI WA JADI

Na Unique Maringo
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi kisutu imeutaka upande wa jamuhuri kuhakikisha taarifa ya upelelezi inakamilika tatika kesi ya kutakatisha fedha na kugushi inayomkabili Rais wa  Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange `Kaburu`

Wakili wa serikali Peter Vitalis na Mwendesha mashtaka wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) Leonard Swai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa alidai upelelezi wa shauri hilo pado haujakamilika.

Hakimu alimtaka Swai kueleza hatua ya upelelezi imefikia wapi ambapo alidai kuwa wamepeleka taarifa   kwaajili ya kupata ripoti ya polisi ambayo wanayoisubiri.

Wakili upande wa utetezi Philemon Mtakyamirwa aliiomba mahakama itoe tarehe ya karibu lakini Swai aliomba kupewa siku 14 kama ilivyo kwa kesi nyingine.

Shauri hilo liliairishwa hadi Agosti 30 mwaka huu kwaajili ya kutajwa.

Kutokana na viongozi hao kurudishwa rumande hadi agosti 30 mwaka huu inamaana hawatapa fursa ya kulishuhudia pambano la watani wa jadi Simba na Yanga linalotarajiwa kupigwa agosti 23 mwaka katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Evans Elieza  Aveva na makamu wake, Geofrey wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha USD 300,000.

Katika shtaka la kwanza, washtakiwa hao wanadaiwa kuwa  walikula njama ya kughushi fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya Machi 15,2016 wakionesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa  USD 300,000 kwa Evans Aveva wakati si kweli.

Katika shtaka la pili alidai kuwa Machi 15,2016 katika benki ya CRDB tawi la Azikiwe Ilala Aveva akijua alitoa nyaraka za uongo ambayo ni fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya Machi 15,2016 wakati akijua ni kosa.

Katika la tatu la kutakatisha fedha, Aveva na Nyange wanadaiwa kuwa kati ya Machi 15 na Juni 29,2016 Dar es Salaam  kwa pamoja walikula njama ya kutakatisha fedha kwa kupata USD 300,000 wakati wakijua ni zao la uhalifu.

Kwa upande wa shtaka la nne la kutakatisha fedha,Aveva anadaiwa kuwa kati ya Machi 15,2016 katika benki ya Baclays Mikocheni alijipatia USD 300,000 wakati akijua zimetokana na kughushi.

Katika shtaka la tano la kutakatisha fedha, mshtakiwa Nyange anadaiwa kuwa  Machi 15,2016 katika benki ya Baclays tawi la Mikocheni alimsaidiaAveva  kujipatia USD 300,000 wakati akijua fedha hizo zimetokana na kughushi.

Washtakiwa wapo rumande kwa sababu shtaka la kutakatisha fedha linalowakabili halina dhamana. ya Machi 15,2016 wakati akijua ni kosa.

Katika la tatu la kutakatisha fedha, Aveva na Nyange wanadaiwa kuwa kati ya Machi 15 na Juni 29,2016 Dar es Salaam  kwa pamoja walikula njama ya kutakatisha fedha kwa kupata USD 300,000 wakati wakijua ni zao la uhalifu.

Kwa upande wa shtaka la nne la kutakatisha fedha,Aveva anadaiwa kuwa kati ya Machi 15,2016 katika benki ya Baclays Mikocheni alijipatia USD 300,000 wakati akijua zimetokana na kughushi.

Katika shtaka la tano la kutakatisha fedha, mshtakiwa Nyange anadaiwa kuwa  Machi 15,2016 katika benki ya Baclays tawi la Mikocheni alimsaidiaAveva  kujipatia USD 300,000 wakati akijua fedha hizo zimetokana na kughushi.

Washtakiwa wapo rumande kwa sababu shtaka la kutakatisha fedha linalowakabili halina dhamana.

No comments