AJIBU AANZA KUCHEKA NA NYAVU

Timu ya soka ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Mlandege ya Zanzibar katika mchezo wa kirafiki uliyopigwa kwenye uwanja wa Amani.

Yanga ilijipatia bao la kwanza kunako dakika ya 49 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wake Ibrahimu Ajibu kabla ya Emmanuel Martine kufunga bao la pili katika dakika ya 73.

Yanga iko Zanzibar ikiendelea na maandalizi ya kujiwinda na pambano lao la ngao ya jamii dhidi ya Simba litakalopigwa agost 23 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Baada ya mchezo huo kikosi cha Yanga kitaelekea kisiwani Pemba kuweka kambi kabla ya kurejea jijini Dar es salaam siku mbili kabla ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani wa hali juu.

No comments