KOCHA MTIBWA SUGAR ASEMA SIMBA IMEMPA MWANGA

Kocha mkuu wa timu ya Mtibwa Sugar,Zubeiry Katwila amesema kwamba mchezo wa kirafiki waliocheza na timu ya Simba una faida kubwa kwake kwani ameweza kuona ubora na mapungufu ya maingizo mapya katika timu.

Katwila alisema kwamba kupitia mchezo huo waliofungwa kwa bao 1-0 amebaini mapungufu ambayo atayafanyia kazi ili kikosi kiweze kufanya vizuri katika michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao.

Alisema kwamba kikosi chake kina wachezaji wengi wapya hivyo kupata mechi kubwa kama ya Simba pamoja na kufungwa lakini kuna kitu wachezaji wamekipata.

Mtibwa Sugar katika mechi hii leo ilifungwa goli 1-0 dhidi ya Simba,bao ambalo limefungwa na Emmanuel Okwi,lakini licha ya kufungwa kwa bao hilo moja kikosi kilifanikiwa kuonyesha hali ya kujiamini kwa muda wote wa mchezo.

No comments