COSTANTINO PIUS ATAMBA KUIPELEKA INJILI VIJIJINI

Muimbaji anaekuja kwa kasi katika nyimbo za injili Costantino Pius ametamba kufanya vizuri kwenye muziki huo na kuhakikisha kuwa analeta mapinduzi kwa waimbaji wa nyimbo hizo.

Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPORT,Pius alisema kwamba dhamira yake ni kuihubiri injili ifike hadi vijijini ambapo anaamini sehemu hizo kumekuwa na mwitikio mdogo hivyo kufika kwake kutaleta chachu ya mafanikio ya wadau kuifahamu vyema injili.

Muimbaji huyo anaetamba na wimbo wake mpya unaojulikana kwa jina la viwango vingine alisema kwamba kuanzia sasa wakati wowote anatarajia kuachia video ya wimbo wake ili jamii iendelee kumfahamu vizuri kwa kile anachokifanya.

Alisema kwamba kwa sasa ameshakamilisha idadi ya nyimbo tatu ambayo ya kwanza inajulikana kwa jina la Siwezi bila yesu ambayo ilianza kumpa mwanga kabla ya kuachia nyimbo ya pili ijulikanayo kwa jina la  Mungu wa miungo ambayo imepokelewa vizuri zaidi na wadau wa nyimbo hizo kabla ya kuachia huu watatu unaotamba kwenye radio uitwao Viwango vingine.

No comments