HIMID MAO ASEMA HAYA KUHUSU YEYE KUJIUNGA NA YANGA

Huku kukiwa na taarifa kwamba klabu ya Yanga iko mbioni kunasa saini ya kiungo wa timu ya Azam FC,Himid Mao kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo katika msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara na michuano ya kimataifa,leo hii mchezaji husika amesema kwamba taarifa hizo si za kweli kwani hajawai kuzungumza na Yanga.

Mao alisema kwamba taarifa hizo anazizisikia kupitia mitandao lakini yeye na meneja wake bado hawajazungumza na uongozi wa Yanga kuhusiana na maswala ya usajili.

Alisema kwamba yeye kwa sasa bado ni mchezaji wa Azam ingawa ameshindwa kuweka bayana juu ya ukomo wa mkataba wake hivyo klabu itakayomuhitaji lazima ifuate taratibu husika ikiwemo kuzungumza na meneja wake.

Hata hivyo MWANDIKE.BLOGSPORT inatambua kuwa kuna mazungumzo yanaendelea kufanywa kati ya uongozi wa Yanga na meneja wa mchezaji huyo ili asaini kandarasi ya kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania bara na taarifa zinaeleza mazungumzo hayo yanaenda vizuri.

No comments