SIMBA WAAMUA KUREJEA KWA DONALD NGOMA

Mashabiki na wanachama wa timu ya Simba bado hawaamini kama mchezaji Ibrahim Ajibu amesajiliwa na klabu ya Yanga kwa ajili ya kuitumikia msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania.

Mwenyekiti wa tawila Simba la Mpira Pesa, Ostadh Masoud alisema kwamba bado kwa upande wao hawaamini juu ya usajili huo wa Ajibu kwenda kwa wapinzani wao hadi hapo atakapotangwazwa rasmi.

Aidha Masoud alisema kwamba endapo kama mchezaji huyo amesajiliwa na Yanga basi ni vyema uongozi ukafanya mchakato wa kulipiza kisasi kwa kumsajili Donald Ngoma ili aweze kuziba nafasi ya Ajibu.

No comments