MALINZI ATAKIWA KUACHIA NAFASI MOJA YA UONGOZI

Baraza la michezo Tanzania BMT,limebaliki mchakato wa uchaguzi wa TFF unaotaraji kufanyika agost 12 mwaka huu uendelee kama kawaida lakini kwa kufuata maagizo yao waliyowapa.

Katibu mkuu wa BMT,Mohamed Kiganja alisema kwamba baraza hilo lilikubali ombi la TFF baada ya kuomba jambo hilo lifanyeke haraka Zaidi kwa ajili ya manufaa ya mpira wa miguu hapa nchini.

Kiganja alisema kwamba,moja ya maagizo ambayo wamewapa TFF ni pamoja na kuwakumbusha wagombea wote kupitia sheria na kanuni za baraza la michezo ili kuendanana na matakwa ya kanuni za baraza hilo.

Alisema kwamba maagizo hayo pia yanaelekeza kwa wagombea kutokuwa na nafasi mbili za uongozi wa mpira ambapo wamewataka viongozi watakaoshinda kubadilisha kanuni hiyo inayoidhinisha mtu mmoja kuwa na wadhifa sehemu mbili.

"Mtu mmoja hawezi kuwa na nafasi mbili za uongozi mfano awe kiongozi wa klabu ama chama huku pia awe kiongozi TFF,hilo jambo hatulitaki na tumeliagiza walifanyie kazi hivyo kwa watakaoshinda waelewe hilo na kama wana nafasi mbili basi moja waiache"alisema Kiganja.

Kauli hii itawabana zaidi viongozi wa vilabu vya Simba na Yanga ambao wengi wao walikuwa na nafasi mbili katika klabu na TFF pamoja na Rais anaemaliza muda wake Jamali Malinzi aliye na nafasi mbili ya TFF na kuwa mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Kagera.

No comments