MSUVA AMLILIA HARUNA NIYONZIMA

Winga mwenye kasi zaidi katika timu ya soka ya Yanga,Simon Msuva amesema kwamba kuondoka kwa Haruna Niyonzima ndani ya klabu hiyo kumemuumiza kwa upande wake kwani kwake Niyonzima alikuwa zaidi ya rafiki kutokana na mambo yao waliyokuwa wanayafanya.

Msuva alisema kwamba alikuwa na mazoea zaidi na mchezaji huyo hivyo atakumbuka vitu vingi kwake, lakini haina jinsi kwani kwake amefanya maamuzi ambayo anaamini huenda yakawa mazuri katika mustakabali wa maisha yake.

"Unajua katika timu lazima kuwe na mazoea,mimi Haruna nilimzoea,nilimzoea kupitiliza kwa hiyo hii habari ambayo imetokea kuwa amesaini si timu nyingine sijui Simba mi sifahamu lakini kwa upande wangu kama amesaini kweli nimeumia lakini pia ni maisha yake yeye na familia yake"alisema Msuva.

Alisema kwamba licha ya kuondoka kwake lakini bado ana imani na wachezaji waliosalia ndani ya Yanga kama kina Thabani Kamusoko ambao anaamini wataendelea kufanya vizuri zaidi katika timu na atashirikiana nao kwa kiwango kikubwa.

No comments