MAYAY NA MTEMI RAMADHANI WACHUKUA FOMU KUWANIA UONGOZI WA TFF

Wachezaji wa zamani waliowai kuwika katika vilabu mbalimbali vya hapa nyumbani pamoja na timu ya Taifa,Ally Mayay pamoja na Mtemi Ramadhani leo hii wamejitokeza katika ofsi za TFF kuchukua fomu za kuwania nafasi ya uongozi katika shirikisho hilo.

Wachezaji hao wakongwe walisindikizwa na wachezaji wenzao wa zamani ambao pia walitamba katika vilabu mbalimbali kwa nderemo na bashasha hadi kwenye ofsi za TFF.

Ally Mayay kwa upande wake yeye amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Rais wa shirikisho hilo akitaraji kuchuana na wagombea wengine akiwemo Rais Jamali Malinzi anaemaliza muda wake wa uongozi.

Mayai alisema kwamba kwa sasa hawezi kuzungumza kwa undani nini ambacho kimemshawishi hadi akaamua kuchukua fomu ya kuwania uongozi kwa kuwa si kipindi cha kampeni bali wakati utakapofika atazungumza kwa undani malengo yake.

No comments