SASA RASMI HARUNA NIYONZIMA NI MALI YA SIMBA

Mjadala wa mchezaji Haruna Niyonzima hii leo umezimwa rasmi baada ya uongozi wa klabu ya Yanga kuwaambia mashabiki na wanachama wake kuwa hawatakuwa na mchezaji huyo katika msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara baada ya kushindwana katika mslahi juu yab kuongeza mkataba mpya baada ya huu wa sasa kuelekea kikomo.

Katibu mkuu wa Yanga,Charse Boniphace Mkwasa amesema kwamba ni kweli walikuwa na dhamira ya kuendelea kuwa na Haruna Niyonzima kwa sababu alikuwa mchezaji tegemeo lakini inashindikana kuwa nae kwa sababu ya kifedha ambapo Niyonzima alihitaji dau kubwa lililowashinda viongozi.

Niyonzima kwa muda mrefu alikuwa gumzo midomoni mwa wapenda soka hasa kila mmoja akihitaji kufahamu wapi anaelekea katika vilabu vya Simba na Yanga ambao ni mahasimu wa jadi.

Hata hivyo taarifa za awali zinaeleza kuwa Niyonzima msimu ujao ataonekana katika klabu ya Simba baada ya kusainii kandarasi ya kujiunga na klabu hiyo kwa dau kubwa la fedha.

CHINI TAARIFA RASMI YA KLABU

TAARIFA KWA UMMA
Klabu ya Yanga SC kupitia kwa Katibu Mkuu Boniface Mkwasa inapenda kuwajulisha wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga juu Mchezaji raia wa Rwanda Haruna Niyonzima ambaye amekua Mchezaji wetu kwa misimu 6 mfululizo katika kiwango cha juu.
Hata hivyo Haruna Niyonzima bado ana mkataba mpaka mwezi Julai na Yanga Sc, lakini hatutaweza kuendelea kuwa nae kwa msimu ujao kwani hatukuweza kufikia mwafaka katika mazungumzo yetu na yeye licha ya timu yetu kuwa na nia za kuendelea nae kwa misimu miwili ijayo.
Klabu inamtakia kila la kheri katika maisha yake na soka kwa ujumla.
Imetolewa na Idara ya Habari na Maelezo
Young Africans Sports club.
21-06-2017.

No comments